Ukiinuliwa Tulizana

Masimulizi …

by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Alitokea panya mmoja kwenye kijiji cha jirani. Panya huyo alimeza kipande cha dhahabu cha mwenye nyumba ya jirani. Mwenye nyumba hiyo alipogundua kuwa dhahabu yake ilikuwa imemezwa na panya aliamua kumtafuta mwindaji ili amtafute yule panya na kumwua ili aipate dhahabu yake. Kitendo hicho cha mwindaji kumtafuta panya kiliwashangaza sana wanakijiji kwa sababu panya walikuwa wengi pale kijijini kwao na walikuwa wanaishi kwenye mkusanyiko na hivyo kuwa pamoja daima. Walijiuliza, mwindaji atamtambuaje huyo panya? Lakini katika hali isiyo ya kawaida alitokea panya moja ambaye alianza tabia ya kujitenga tenga na panya wenzie. Hivyo mwindaji alipofika wala hakupata shida kabisa kwani moja kwa moja alimlenga yule panya ambaye alikuwa hachangamani na wenzie. Mwindaji na mwenye nyumba walimpasua yule panya na kweli wakakuta kile kipande cha dhahabu. Mwenye nyumba alishangaa na kufurahi sana. Hatimaye alimuuliza mwindaji kwamba alijuaje kama ni huyo panya aliyemeza ile dhahabu? Mwindaji alimjibu kiurahisi sana kwa kusema: “wapumbavu wakipata utajiri huwa hawapendi kujichanganya na wenzao. (When stupid people get rich they don’t mix with others) Somo lingine la nyongeza na la busara ni kwamba ukifanikiwa au ukibarikiwa kupata utajiri inakupasa uache majivuno ama majigambo. Ni vema ukabaki kama vile ulivyokuwa mwanzo. Utu wako utabakia kuwa wa thamani mbele za watu.



The Healing Hands Project

We are excited to launch the #HealingHands project. The project supports interpersonal counseling, group talk therapy and psychoeducation resources to be delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. It also promotes the economic growth of grandmothers who are trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program #mhGAP. Income generated from sales of the jewelry will also support the sustainable implementation of accessible psychosocial interventions among underserved communities. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay posted.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #ArtTherapy

Previous
Previous

Kikulacho Ki Nguoni Mwako

Next
Next

Mdharau Mwiba Guu Huota Tende