Anza na Kidogo

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi ...

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Palikuwa na binti mmoja ambaye alihitimu chuo kikuu na alifaulu vizuri sana. Lakini kutokana na shida ya ajira aliamua kuanza biashara ya kwenda feri soko la samaki ili kununua samaki kwa ajili ya kukaanga na kuuza kwa wateja. Alianza kazi hiyo kwa furaha na amani tele japo wasomi wenzie walikuwa wanamkejeli na kumcheka sana. Kejeli zao zoligonga mwamba, kwani hakujali na hakubabaishwa na hilo kabisa. Aliendelea na biashara yake wakati wenzie walikuwa wanatembea kutwa na bahasha zao zenye vyeti vya shahada mkononi kwa lengo la kutafuta kazi.

Mwisho wa siku yule dada alipata mtaji na akaanza kwenda China kuchukua bidhaa na wakati huo huo akawa amefungua duka kubwa na akaweza hata kuwaajiri wenzake aliosoma nao. Hadi leo hana mpango wa kazi za kuajiriwa na maisha yake yanaendelea kuwa mazuri kila uchao.

Tunajifunza nini kutoka kisa hiki? Hadithi hii inatufundisha yafuatayo:

  1. Usomi wetu usitufanye tuchague kazi hadi tunapitiliza na mwisho tukailaani hata ile elimu tuliyopata;
  2. Ubunifu na kujituma ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu. Tuitumie elimu tuliyoipata kutafuta kazi mbadala ya zile tulizokuwa tunategemea baada ya kumaliza masomo yetu na kupata shahada;
  3. Mwisho, ikumbukwe kuwa kila jambo lina mahala pa kuanzia, hakuna miujiza. Tunaaswa kuanza na kidogo ili hatimaye tuweze kufika juu kwenye ushindi.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Kawaida Ni Kama Sheria

Next
Next

Ukiona Mwenzako Ananyolewa, Na Wewe Tia Maji