Mkataa Pema, Pabaya Panamwita

Susan Njana - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi ...

by Susan Njana (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Simulizi hii inamhusu dada mmoja katika kijiji kimoja ambaye alibahatika kupata fursa nzuri ya kupata mafanikio katika maisha yake. Kwa bahati mbaya aliikataa fursa hiyo akitegemea kupata nafasi nyingine nzuri zaidi pamoja na kwamba alikuwa hana uhakika wa kuipata nafasi nyingine.

Dada huyo alichumbiwa na kaka mmoja lakini alijiona ni mzuri sana na kwamba hawezi kuolewa na kaka huyo ambaye alikuwa akifanya kazi ya ukarani tu katika ofisi moja ya serikali. Alimponda sana huyo kaka kwani alimwona ni mwenye sura isiyovutia na pia kipato chake ni duni.

Kijana huyo alipokataliwa na huyo dada mwenye kujisikia alimfuata dada mwingine aliyemfahamu katika kijiji kile kile na kumwomba awe mchumba wake. Dada huyo mwingine hakusita akamkubali na kuanza mahusiano hadi ndoa ikafanyika kanisani. Walianza maisha, Mungu akawajalia kupata watoto. Kwa bahati nzuri huyo kijana alipata nafasi ya kwenda kwenye masomo ya kujiendeleza. Maendeleo yake yalikuwa mazuri, alipata shahada ya kwanza na ya pili pia kwa muda mfupi.

Baada ya masomo alipandishwa cheo na kuwa Afisa Utumishi Mkuu. Maisha yalibadilika na kuwa mazuri kutokana na maslahi kuongezeka.

Kwa upande mwingine, yule dada aliyekataa kuolewa naye alibaki hivyo hivyo bila mume na mbaya zaidi akajiingiza kwenye ukahaba na ulevi. Hali yake ilianza kuchuja haraka, akakosa heshima kijijini na hata matarajio yake ya kuolewa yakatoweka kabisa. Matokeo yake akapewa mimba na kijana asiyekuwa na uwezo wa kutunza familia. Ndoto zake za kupata maisha mazuri ziliishia hapo.

Watu hapo kijijini walimcheka kwa yaliyompata, walimpa majina ya kejeli, jina la " Fungu la kukosa" kwa maana alikuwa amebahatika kupata mchumba mwema akamkataa. Maisha ya yule kaka na mke wake yalikuwa ni ya maelewano mema na yenye mafanikio endelevu. Maisha ya yule dada aliyeitupa bahati ya kuolewa yakawa magumu na yasiyo na matumaini tena.

Ama kweli, "mkataa pema pabaya panamwita." Inabidi tujifunze, tuache dharau kwani kila mtu ana fungu lake, huwezi jua huyo unayemkataa amewekewa fungu gani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Tuwashirikishe Watoto Kazi Za Shamba Kwa Mafanikio

Next
Next

Kawaida Ni Kama Sheria