Ukimtendea Wema Mwenzio Kuna Siku Mungu Atakukumbuka

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Masimulizi ...

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Siku moja mwanamke mjane mwenye maisha ya kwawida tu alipata changamoto ya mahitaji ya nyumbani kwake. Huyu mwanamke alikuwa mcha Mungu sana, muombaji mzuri na mshiriki mzuri sana kwenye matukio ya kanisani.

Kuna Jumamosi moja alitakiwa kwenda kwenye kongamano ambalo lilikuwa ni kanisa tofauti na like ambalo huwa anasali. Lakini hakuwa na nauli ya kutosha. Nyumbani karibu vyakula vyote vilikuwa vimeisha. Alikuwa katika hali ngumu. Akawaza atafanyeje na hiyo hali. Kwa vile alikuwa ni mama mwenye imani kubwa kwa Mungu alijua kuwa atafanya njia. Hivyo aliondoka nyumbani kwenda kwenye kongamano.
Alijitahidi kubana fedha kidogo aliyokuwa nayo kwa kupanda basi moja badala ya mawili na pia aweze kubaki na fedha kidogo ya kutoa sadaka na nauli ya kurudia nyumbani. Alivyofika kanisani akaendelea na ratiba mpaka mwisho bila kuonesha dalili za kuwa na shida. Ilipofika mwisho wa kongamano wakina mama wengi waliondoka, yeye alibaki na mwenzake getini wakiongea.

Mara akatokea mlemavu wa macho kwa bodaboda na kumuacha pale. Yule mwanamke alipomuona yule mlemavu anatafuta mlango akamkimbila na kumshika mkono akamuuliza: “una shida gani baba?” Akajibu: “nimekuja kanisani, je hapa ni kanisa la Pentecoste”?Yule mama akamjibu: “Hapana, sio hapa. Umelipita kule ulikotoka”. Boda boda ilikuwa imeishaondoka.

Yule mama mcha Mungu alimuaga mwenzake pale getini ili aweze kwenda kumsaidia yule baba mlemavu wa macho na kumpeleka kule kanisani ambako kulikuwa na umbali wa kama hatua 300 hivi. Alipomfikisha alimkabidhi kwa wahusika wa pale kanisani. Kumbe yule baba alikuwa anaenda kuombewa. Yule baba akamshukuru yule mwanamke kwa kumsaidia. Basi yule mwanamke akaanza naye safari ya kurudi kwake.

Alipofika nyumbani msichana wa kazi akamwambia kuwa walikuja wageni mke na mume. Yule mama akamuuliza watu hao walitoka wapi. Akamjibu: “ni wifi yako wa Salasala na ameleta vitu viko stoo, mchele kilo 10, sukari kilo 5, na mafuta ya kula lita 5. Yule mwanamke alimshukuru Mungu kwa matendo yake makuu. Pia akatambua kuwa kwa kumsaidia yule baba Mungu amemkumbuka na kumsaidia shida aliyokuwa ameiacha nyumbani kwake kabla hajaenda kanisani. Alimpigia simu wifi yake na kumshukuru.

Tunachojifunza hapa ni kuwa na upendo na utayari wa kumsaidia kila mtu bila kujali hali ya mtu. Kuwasaidia wenzetu katika masuala yaliyo ndani ya uwezo wetu ni uungwana ambao tutalipwa wakati na sisi tutakapopata matatizo. Tuwekeze katika maisha yetu kwa kuwasaidia wenzetu walio katika shida, tutalipwa huko mbeleni.

 

The Healing Hands Project

The Healing Hands project will economically empower people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community - eliminating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain the implementation of accessible psychosocial interventions in underserved communities and promote the economic empowerment of the grandmothers who have been trained in and are implementing WHO's mental health Gap Action Program. Healing Hands provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources delivered through arts, where clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection to stay up-to-date.

#MentalHealth #Grandmother #Wisdom #Wellness #mhGAP #HealingHands #Art #Culture #Tanzania

Previous
Previous

Tusitumie Njia Ya Udanganyifu Kwa Kujipatia Mali

Next
Next

Tuwashirikishe Watoto Kazi Za Shamba Kwa Mafanikio