
Bidii Ina Tabia Ya Kumtabulisha Mtu.
Watu wengi tunafanya mambo lakini hatuyafanyi kwa bidii, tunafanya ili mradi tu yafanyike. Unaenda kazini lakini huna bidii ya kwenda kazini, leo unaenda kesho hauendi. Kila siku unaenda ukiwa wa mwisho na unatoka ukiwa wa kwanza.

Zuia Mawazo Hasi.
Upo ule wakati kwenye maisha yako unaona kama umefika mwisho kabisa.Yaani, kila ukijiangalia unaona kabisa hauna nguvu tena za kuendelea mbele.

Jitie Moyo Kila Wakati!
Haijalishi unapitia changamoto gani kwenye maisha yako, jitahidi kupata muda wa kujipa moyo. Kama ni chakula kula vizuri mlo kamili ili usiidhuru afya yako halafu ukasababisha magonjwa sugu.Pia pata muda wa kujijali yaani jipendezeshe kuoga na upake mafuta yako ung'are na uvae vizuri.

Usifanye Maamuzi Kwa Ajili Ya Leo Tu, Angalia Na Kesho Yako.
Usibamize mlango wakati wa kuondoka. Ukifunguliwa na mtu /watu mlango uliouhitaji siku ukitaka kuondoka usiubamize huo mlango kwa nguvu , huenda kesho ukahitaji kuutumia tena wakati wa kuingia.

Tone La Maarifa.
Ukitaka kufanya vizuri maishani wafanyie watu yaliyo mazuri, kwa sababu hakuna namna yoyote ambayo unaweza ukafanikiwa pasipo watu.

Fanya Maamuzi Ukiwa Na Utulivu.
Usifanye maamuzi ukiwa na njaa kali au pochi yako iko tupu. Pale utakaposhiba, utajuta.

Endelea Kujaribu.
Ni kawaida kabisa kwa mtoto anapotaka kuanza kusimama kushika na kuegemea kila kitu ili kimsaidie asimame. Wakati mwingine anaweza hata kuegemea vitu vya hatari, kama vile chupa ya chai, jiko la moto na vingine vingi tu vinavyokuwa karibu yake. Kwa ujumla, anaweza kushika kitu chochote ambacho kinaweza kuwa ni cha hatari ili mradi tu asimame.

Mafanikio Ya Ushirikiano
Ushirikiano ni mbinu ya kukuwezesha kumudu maisha mahali popote na ukiwa na mtu yeyote. Ushirikiano unahusisha pande mbili, yaani unatoa ushirikiano na unapokea ushirikiano, kwa hiyo unapojenga ushirikiano sio tu unanufaika mwenyewe peke yako, bali mnanufaika nyote , yaani pande zote mbili.

Muda Ni Mali
Matumizi ya muda wako yanaweza kukunufaisha na kukutoa hatua moja kukupeleka hatua ya juu zaidi ya maisha.Au matumizi ya muda wako pia yanaweza yakawa ni hasara kwako. Muda ni mali, tunaulinganisha na fedha.

Tatizo Huzaa Faida.
Tatizo ni tatizo, liwe la afya au la uchumi, mwisho wake litazaa faida. Hata likiwa ni tatizo la madeni, bado nalo litazaa faida. Kila tatizo lako litazaa faida katika maisha yako kwa sababu, kila tatizo lililo mbele yako, katika hali ya kawaida, utalifanyia kazi na mwisho kutakuwa na faida.

Ili Upokee Unahitaji Maandalizi
Baadhi ya vitu kwenye maisha yako utachelewa kuvipata. Kuchelewa huko, haina maana kuwa Mungu hataki uvipate, bali ni kwa sababu Mungu anakupa muda wa kujiandaa kwanza.

Kila Mtu Ana Mfariji Wake
Kwenye kila majira ya maisha yako, kuna mtu anakuwa ameandaliwa kuwa mfariji wako. Mtu huyu anakuwa amepewa moyo wa kukuonea huruma ya kipekee na huwa yuko tayari kutumia muda wake kukufariji.

Kujifunza Ni Kila Siku
Kama unatamani kuwa vile unataka kuwa, jitahidi uvuke kawaida ya mfumo unaozaa wale wanaokuvutia.Kama unataka kuwa mtu uliyefanikiwa zaidi ya wale unaowaona wamefanikiwa, jitahidi mno uvuke kawaida, ili uende zaidi ya pale walipoishia.

Umdhaniaye Siye
Katika maisha, wengi wetu tunaangalia sana matendo ya mwanadamu kwa juu juu, bila kutafakari kwa undani mazingira halisi au asili ya mtu huyo. Mara nyingi jambo hili linajitokeza kwa watu ambao wameishi na kuaminiana kwa vile kila jambo linaenda vizuri na pia hapajawahi kutokea kasoro yoyote kati yao.

Weka Bajeti Upate Mafanikio
Kuna umuhimu wa kuwa na bajeti unapoanza au unapoendesha mradi wowote. Ili uweze kuidhibiti pesa ni lazima kuwa na bajeti. Ni muhimu kuwa na bajeti kwani itakusaidia kukuonesha pesa inatoka wapi na inakwenda wapi.

Achana na Neno Haiwezekani Upate Mafanikio
Ukitaka kupata mafanikio maishani mwako usiwe na mazoea ya kutumia neno ‘haiwezekani’. Mojawapo ya udhaifu mkubwa wa binadamu ni kuzoea kutamka neno hili la haiwezekani. Mara nyingi watu wenye neno haiwezekani midomomi mwao ndio ambao huwa hawafanikiwi katika maisha.

Mpe Adui Yako Tabasamu Badala Ya Machozi
Unaporuhusu uchungu na maumivu ndani yako ni rahisi sana kuchoka na kukataa tamaa. Usibebe kila kitu, na wala usichukulie kila kitu kwa uzito, utaelemewa.

Kubali Kupoteza Ili Uende Viwango Vingine
Katika maisha unaweza kupoteza nafasi, au watu uliowaamini sana. Pengine hata uliweza kufikiri kuwa bila wao maisha au malengo yako hayatafanikiwa.

Jielewe Kwanza Mwenyewe, Watakuelewa Pia
Kama unataka kuwa kitabu cha kusomwa hata na vizazi vijavyo, hakikisha unajisoma na kujielewa mwenyewe, kwanza kwa mawazo yako na ujumbe wako. Ila kama unataka kuwa kitabu cha kusomwa leo na baadae kusahauliwa, basi endelea kutafuta kueleweka na watu wa leo.

Tuwe Wastaarabu Na Busara Katika Maongezi
Binadamu tunatakiwa kuishi kwa kufuata taratibu fulani zilizopo kwenye jamii, hii ni pamoja na jinsi tunavyozungumza na wenzetu. Kwa maana hiyo, ukiwa mstaarabu na mwenye busara huwezi kuuliza uliza watu maswali ambayo hayastahili kuulizwa, maswali kama: ‘Bado hujaolewa tu?….Una watoto wangapi?…Utazaa lini?…Mbona umri umeenda?…na mengine mengi.