Muda Ni Mali

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Matumizi ya muda wako yanaweza kukunufaisha na kukutoa hatua moja kukupeleka hatua ya juu zaidi ya maisha.
Au matumizi ya muda wako pia yanaweza yakawa ni hasara kwako. Muda ni mali, tunaulinganisha na fedha.

Ukiwekeza muda wako vizuri, utaona faida yake, kwa maana matumizi yake yana uhusiano wa moja kwa moja na faida inayopatikana.
Tofauti iliyopo kati ya muda na fedha ni kwamba muda ukipotea haurudi lakini fedha ikipotea, unaweza kupata nyingine tena maradufu kuliko uliyokuwa nayo hapo awali.

Mfano halisi ni pale tunaposema, hatuwezi kuununua mwaka uliopita, mwaka ukishapita hauwezi kurudi. Lakini kwa bahati mbaya umepoteza fedha Sh. 10,000, mtu anaweza kukupa 10,000 ili kuziba pengo lako la Sh. 10,000 uliyopoteza.

Nahitimisha kwa kusema kwamba fedha inaweza kurudi lakini muda haurudi asilani, yatupasa tuutunze.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Mafanikio Ya Ushirikiano

Next
Next

Kichwa Pasipo Ufahamu, Ni Mzigo Wa Shingo.