Mafanikio Ya Ushirikiano

Victoria Nakajumo - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Ushirikiano ni mbinu ya kukuwezesha kumudu maisha mahali popote na ukiwa na mtu yeyote. Ushirikiano unahusisha pande mbili, yaani unatoa ushirikiano na unapokea ushirikiano, kwa hiyo unapojenga ushirikiano sio tu unanufaika mwenyewe peke yako, bali mnanufaika nyote , yaani pande zote mbili.

Ushirikiano ni mfano wa kupanda mbegu ambayo itakurudishia matunda. Katika ushirikiano, ni vema usiwe tu ule wa aina ya mdudu aitwaye kupe,?wa kunyonya wenzako, bali ni ule wa nipe nikupe. Hata anayetoa msaada bure, kuna anachorudishiwa, hata kama siyo kutoka kwa binadamu mwenzie, basi hata Mungu atakurudishia.

Tuchukue mfano wa timu ya mpira ambapo kila mtu ana kazi yake. Pamoja na kwamba wachezaji wote wanacheza katika timu moja, kila mtu anakuwa na jukumu lake ambalo linafanyika kwa ushirikiano ili kufikia lengo lao.

Hii ina maana kuwa, ili ushirikiano utimie au ukamilike, inabidi uende pande zote mbili. Usiwe ushirikiano unaoegemea upande moja. Inapokuwa hivyo, yaani wa kuegemea upande moja, huo unakuwa siyo ushirikiano bali ni unyonyaji ama ukandamizaji wa upande ulio dhaifu.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection 

Previous
Previous

Shinda Tabia Ya Hasira Katika Maisha Yako

Next
Next

Muda Ni Mali