Kichwa Pasipo Ufahamu, Ni Mzigo Wa Shingo.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

Tukiwa kama walezi tunatakiwa kuwa makini na ulezi tunaofanya kwenye familia zetu. Malezi yanatakiwa kuanza mapema ili kuweza kukuza familia zetu katika taratibu nzuri na salama kwa watoto wetu. Tusipokuwa makini basi watoto wetu watakua katika maisha haya tusemayo ni ya kidigitali. Tunaweza kusema kwamba tunaenda na wakati, mwisho wa siku mzigo utakuja kuwa wa kwetu.

Usemi huu unaendana na ule usemao mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hii ina maana kuwa tusipowalea ipasavyo, hiyo shida tutakuwa tunajipa wenyewe. Yatupasa tuwape watoto wetu
malezi mazuri ili waweze kukua kwa maadili mema yanayokubalika na jamii zetu. Malezi mabaya yatatuletea mzigo sisi wenyewe hapo baadaye,

Mzigo ukiwa mzito itakuwa ni balaa kwetu wazazi. Utafika wakati akifikia umri wa ufahamu, huwezi kumueleza kitu akakuelewa. Tatizo kubwa ni kwamba hukufanya hivyo pale ulipotakiwa kufanya hivyo. Sasa bila ubishi, hilo litakuwa ni zigo lako. Utaishia kulalamika kwa kusema kuwa watoto hawakusikii. Kumbe ni makosa yako mwenyewe. Ni vile ulivyowajenga toka mwanzo wa malezi yao.

Tuseme tu kwamba unapokuwa na watoto ambao hawakusikii ni sawa na kichwa pasipo ufahamu na pia kuwa mzigo wa shingo. Kwa sababu shingo haiwezi kugeuka kama kichwa hakina ufahamu mzuri.
Tujitahidi kuwalea watoto wetu kulingana na maadili yetu. Bila hivyo wataingia kwenye matatizo mengi tu, yakiwemo na yale ya afya ya akili.

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Muda Ni Mali

Next
Next

Usisumbuke Na Wanao Sumbuka Na Wewe!