
Maneno Matupu Hayavunji Mfupa.
Maneno ni matamshi yaliyoandikwa ama yaliyotamkwa kutoka kwenye vinywa vya watu. Mathalani, maneno yanaposemwa juu yako ni budi ukayatafakari kwanza ili ujue yana maana gani. Endapo maneno hayo hayaleti madhara yoyote basi hayatakuwa na shida kwako, shida itakuwa pale tu mtu atakapokushikia silaha na akakudhuru.

Mcheza Kwao Hutunzwa.
Mcheza kwao ni mtu ambaye anajishughulisha sana na mambo yanayofanyika kwenye jumuiya yake. Kutunzwa ni kupewa tuzo/zawadi pale atakapofanikisha jambo. Kiubinadamu huwa ni jambo zuri kutambuliwa mchango wao pale mtu afanyapo vizuri, iwe ni kwenye jumuia, masomo, kilimo ama eneo la kazi. Hata katika familia, inatakiwa zawadi zitolewe kwa wana familia.

Msuli Tembo Matokeo Sisimizi.
Tembo ni mnyama mkubwa kuliko wote waishio porini. Kwa upande mwingine, sisimizi ni mdudu mdogo sana kiasi kwamba usipoangalia kwa makini, unaweza usimuone kwa jinsi alivyo mdogo.

Adui Mwombee Njaa.
Adui ni mwanadamu ambaye hayupo katika upande wa mwanadamu mwenzake yaani asiyekuwa na upendo kwa mwenzie. Njaa ni hali ya kukosa chakula. Sote tunajua kuwa mahitaji muhimu kwa mwanadamu ni chakula, mavazi na mahali pa kuishi. Mavazi na mahali pa kuishi sio muhimu sana ukilinganisha na mahitaji ya chakula kwa sababu bila chakula mtu hawezi kuishi.

Nyakati Ngumu Zisifunue Madhaifu Yako!
Maisha ya mwanadamu yamegawanyika katika maeneo mbalimbali na tofauti. Kipindi cha mpito hakina budi kutokea kwa kila mtu. Hakuna ambaye anaweza kusema hajapitia nyakati ngumu katika maisha yake. Kuna nyakati nyingine unapitia magumu kwa ajili ya kukuvusha na kukupeleka mahali fulani.

Kuugua Siyo Kufa
Kuugua ni hali ya kuwa na ugonjwa, na mtu mwenye ugonjwa hujulikana kama mgonjwa. Mtu anayeugua au mgonjwa hupenda kupata tiba ili aweze kupona. Mara nyingi mgonjwa anapozidiwa, fikra zinazomuujia ni kuwa anaondoka, yaani anakufa.

Hewala Si Utumwa!
Hewala ni neno linalomaanisha "ndiyo" au "ni sawa". Hii ina maana ya kukubali na siyo kulazimishwa kama vile ifanyikavyo kwa watumwa. Mtu anaweza kukubali tu ili wafikie suluhu katika kutokukubaliana kwao au kufikia muafaka kuwa basi na yaishe ili amani tipatikane.

Panapofuka Moshi Pana Moto.
Moshi ni hali ya ukungu wa joto na harufu ya kuunguzwa kwa majani, miti na hata karatasi. Hali hii unaweza kuiona kwa macho pia unaweza kuihisi kupitia kwenye pua. Kwa mfano huwezi kuona moshi unafuka kutoka msituni bila kuwa na moto nyuma yake. Hivyo moto huwa ndiyo sababu ya moshi kufuka.

Inyeshe Tuone Panapovuja
Mvua ni baraka ambayo huwanufaisha watu wote. Mkulima ama mfugaji akinufaika na mvua, mazao yapatikanayo kutoka kwao yatawanufaisha watu wote.

Usiache Tawi Kabla Hujashika Tawi!
Matawi ni sehemu ya mti ambayo huchipua katika mti na ile sehemu inayoshika majani. Ni kawaida ya mtu ambaye anapanda au anashuka mtini kushika tawi, asipofanya hivyo anaweza kuanguka.

Unaweza Kusahau Maumivu Lakini Sio Tukio!
Unaweza ukawa na maumivu fulani kama ni ya ugonjwa au maumivu mengine ya maisha. Maumivu hayo yanaweza kuwa ni ya muda fulani au kipindi fulani tu lakini mwisho yakapata jawabu. Katika hali hiyo unaweza ukasahau tu pindi pale linapokuja kupata majibu. Hapo itakuwa sio rahisi tena kukumbuka kama kuna jambo lilikuwa limekutesa. Mfano mzuri ni pale unapokuwa unaumwa lakini ukipona inakuwa sio rahisi tena kukumbuka maumivu uliyokuwa ukipata.

Jifunze Kutangaza Mema Kwa Ajili Yako.
Mara zote unatakiwa kutangaza mema kwa ajili yako. Kila mara jiambie, mimi sio wa kushindwa kwa sababu sikuumbwa kushindwa.

Maji Yakimwagika Hayazoleki!
Maji huwa yana nguvu sana yakiwa kwenye njia yake. Pamoja na umuhimu mkubwa wa maji kwa viumbe hai, yakimwagika umuhimu wake unakuwa haupo tena maana huwezi kuyazoa na kuyatumia.

Usilie Mbele Ya Adui, Hata Kama Unahitaji Msaada Wake.
Kupata na kukosa ndio maisha ambayo kila binadamu anapitia kila iitwapo leo. Kusaidiana katika shida na raha ndio kiulimwengu. Hapo ndipo tunapoonyesha upendo wetu kati ya mtu na mtu.
Omba Ufahamu Katika Maisha Yako!
OMBA UFAHAMU KATIKA MAISHA YAKOALFREDA GEORGEUfahamu ni kujua kipi ni kizuri kwako na kipi ni kizuri kwa jamii inayokuzunguka.Hali kadhalika, ufahamu ni kujua kipi ni kibaya kwako na kipi ni kibaya kwa binadamu wenzio ili uweze kukiepuka.Mtu yeyote mwenye ufahamu hutembea katika haki. Hata kama kuna jambo baya, atalihukumu katika haki.Katika maisha, inakupasa ujihukumu mwenyewe kwanza pale unapokuwa umekosea. Usisubiri watu wakuhukumu. Watu wengi wana tabia ya kupenda kuhukumu wenzao na sio kujihukumu wenyewe. Hapo ndipo vurugu na kutokuelewana kunapoanzia. Ni kawaida ya wanadamu kupenda kujitetea kwanza. Ukijua kujihukumu katika yale mabaya unayoyatenda, basi utabadilika. Utakuwa mtu wa kuheshimu kila apitae mbele yako.Usipoweza kujihukumu mwenyewe hautakaa ubadilike, zaidi utawachukia wale ambao wanataka ubadilike. Ukweli ni kwamba, ukiwa na tabia hiyo, hautaishia popote zaidi ya kushindwa.Hatua ya kupata ufahamu, huwa ni ngumu sana kuifikia. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna vikwazo vingi vya kukutoa katika ufahamu. Hapo ndipo panahitaji uvumilivu maana mambo mengine yatakuudhi na kukukatisha tamaa.Ukibahatika kupata ufahamu, utakuwa umepata kila unachohitaji katika maisha yako. Kwa kawaida, Mungu humtumia mtu mwenye ufahamu na huyo ndiye atakaye sababisha upate kile ambacho umekuwa ukikitamani siku zote. Ili uwe na maisha mazuri, yakupasa uombe kutunukiwa ufahamu na hapo ndipo utakapopata amani.

Maarifa Na Hekima Ni Bora Kuliko Vitambulisho.
Maarifa na hekima vina thamani sana kuliko hicho unachokitafuta. Ukiwa na ufahamu na hekima una zaidi ya fedha. Hii ni kwa sababu ukiwa na huo ufahamu na hekima utafanikiwa kuwa tajiri. Hekima itakuongoza kupata kila unachohitaji katika maisha yako.

Unakimblia Wapi Unapopatwa Na Jambo?
Yako mambo yanayotokea katika maisha ya mtu pasipo yeye mwenyewe kujua. Mambo hayo yanaweza yakawa mazuri au mabaya lakini pengine yeye haelewi nini kinaendelea.

Utayari Una Faida.
Utayari maana yake ni kujitoa kufanya jambo lililokusudiwa na ndio ufunguo wa maisha. Ni ile shauku ya kutaka kufanya jambo na kuzingatia sawasawa na vile unavyoagizwa.Unapozingatia na kutii, ni lazima utakutana na usitawi wako katika kila jambo unalokusudia.

Njia Ya Muongo Ni Fupi!
Mlimbua nchi ni mtu ambaye anaifahamu sana nchi yake. Kwamaneno ya sasa huyu mlimbua nchi tunasema mhujumu wa nchi yaani anaisema vibaya nchi yake; anatoa siri za nchi yake, anaiweka nchi yake katika hali ya hatari kwa namna yeyote anayotaka yeye.

Tunda Jema Halikai Mtini.
Matunda ni aina ya chakula ambayo hulinda miili yetu na magonjwa mbalimbali. Katika mada hii, tunaongelea juu ya tunda ambalo ni moja kati ya matunda mengi yanayosifiwa kuwa ni mema na mazuri. Hii ni wazi tunda lolote lililo zuri haliwezi kukaa sana mtini maana lazima lichumwe mapema na kuliwa.