Adui Mwombee Njaa.

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Adui ni mwanadamu ambaye hayupo katika upande wa mwanadamu mwenzake yaani asiyekuwa na upendo kwa mwenzie. Njaa ni hali ya kukosa chakula. Sote tunajua kuwa mahitaji muhimu kwa mwanadamu ni chakula, mavazi na mahali pa kuishi. Mavazi na mahali pa kuishi sio muhimu sana ukilinganisha na mahitaji ya chakula kwa sababu bila chakula mtu hawezi kuishi.
Hivyo msemo huu wa adui yako muombee njaa una maana kuwa akipata njaa pasina shaka atakufa. Endapo uadui utafikia hapo pa kuombeana kifo basi ujue hali imekuwa mbaya sana.
Kwa kawaida, hapa duniani huwezi kukosa kuwa na adui kwa sababu watu wengine hawapendi wenzao wafanikiwe. Pale mtu anapoona umefanikiwa, mwingine anaweza kuwa na chuki nawe bila sababu yoyote. Mtu wa namna hiyo ukimjua, usimwonyeshe chuki bali muonyeshe upendo mkubwa ili hatimaye aweze kurudisha moyo na kuwa na upendo kwako. Akuchukiaye mwambie yeye aliyekuleta duniani yaani Muumba wako ana makusudi nawe. Yakupasa umuombe Muumba wako akupiganie ili aweze kuleta upendo kati yenu.
Hapa tunajifunza kuwa na mapenzi kwa adui zetu kwani chuki kwa chuki hazijengi katika maisha. Tupendane kwani maisha ni mafupi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection