Nyakati Ngumu Zisifunue Madhaifu Yako!

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha ya mwanadamu yamegawanyika katika maeneo mbalimbali na tofauti. Kipindi cha mpito hakina budi kutokea kwa kila mtu. Hakuna ambaye anaweza kusema hajapitia nyakati ngumu katika maisha yake. Kuna nyakati nyingine unapitia magumu kwa ajili ya kukuvusha na kukupeleka mahali fulani.
Kubwa ambalo unatakiwa kulijua ni kwamba usikubali nyakati ngumu zikutoe kwenye mstari wa mipango yako.
Hali kadhalika, si vema unapopitia kwenye magumu kutangaza changamoto zako kwa watu. Binadamu wengine hawaaminiki. Siyo kwamba kila utakaemuambia atakuwa wa msaada kwako. Hata huyo unayemweleza naye anayo mengi tu anayoyapitia, na pengine ni zaidi ya hayo yako.
Unashauriwa kuwa katika kipindi hicho utulie na umuombe Muumba wako akusaidie. Usitegemee msaada wakati wa nyakati ngumu, kwani unaweza usifanikiwe. Na pengine, changamoto zako zinaweza kukuangamiza pale unapoamua kuwashirikisha watu. Kwa kupitia hayo, wengine wanaweza wakatumia changamoto zako kama fimbo ya kukuangamiza zaidi.
Kama binadamu, yakupasa ukomae na hali yako huku ukiwa na matumaini ya kutoka kwenye hilo tatizo. Hata kama unapitia magumu, usijionyeshe kwa watu, wanaweza wasikusaidie kwa lolote. Kumbuka kuna watu wakifahamu jambo lako hata kama lilikuwa linakaribia kwisha, wanaweza wakafanya lisiishe au hata wakalikuza na likawa kubwa zaidi ya lilivyokuwa awali.
Cha msingi, usikate tamaa, endelea kupambana hadi uvuke. Maisha ndivyo yalivyo, maisha ni mapambano.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection