Samaki Mkunje Angali Mbichi!

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Samaki ni kiumbe kinachoishi majini. Mara baada ya kuvuliwa, baadhi ya samaki hutakiwa kukunjwa kwa ajili ya kuhifadhiwa au kwa matumizi ya baadaye. Ili huo mchakato uende vizuri ni lazima samaki hao wakunjwe kulingana na mahitaji ya mlaji. Endapo samaki atakawizwa kukunjwa mara baada ya kuvuliwa, huharibika kiasi kwamba hataweza kukunijka tena.
Vivyo hivyo, hata kwa binadamu, ukitaka kufanya jambo lako, hakikisha unalishughulikia mapema bila kuchelewa kwani kwa jinsi unavyochelewa, ndivyo mambo yanavoyoweza kuharibika. Ikifikia hatua hiyo utajikuta huwezi kufanya hilo jambo tena.
Mfano mzuri ni wa mtoto ambaye amedekezwa na wazazi wake. Mtoto huyu hapewi fursa ya kufanya kazi za nyumbani k.m. kufua nguo zake, kupika, kulima, kuosha vyombo au kufanya usafi. Mtoto huyo akienda shule ya bweni hupata shida sana kujihudumia kiasi kwamba anaona kuwa anaonewa, anateswa na kunyanyaswa. Hali yake hubadilika na matokeo yake huwa ni kufeli.
Vivyo hivyo, baadhi ya wasichana hushindwa kukaa kwa waume zao kutokana na ile tabia waliyoizoeya ya kufanyiwa kazi zote na wasichana wa kazi wakiwa kwa wazazi wao. Mwisho wake huwa ni kuachika.
Kutokana na simulizi hii inatupasa tuache kuwalea watoto wetu kama mayai ambayo huvunjika yakiwekwa vibaya. Yatupasa tuwalee watoto bila kuwadekeza ili waweze kujitegemea wakati hatupo.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection