Asiyekubali Kushindwa, Si Mshindani!

Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwa kawaida kuna mashindano ya aina mbali mbali katika nyanja tofauti tofauti kulingana na mazingira ya sehemu husika.
Mtu yeyote anapoingia kwenye mashindano yoyote yale hutegemea kushinda. Lakini inapotokea ameshindwa, hulalamika au kuona kuwa kaonewa. Anasahau kuwa katika mashindano kuna mshindi na mshindwa. Mara zote mshindi huwa ni mmoja tu.
Hivyo katika maisha, jambo lolote likikushinda, yakupasa ukubali kuwa umeshindwa. Cha msingi, usikate tamaa katika maisha, wewe endelea kujaribu tena na tena. Pale unaposhindwa, unatakiwa kukubali matokeo. Inakupasa ujipe moyo na ujipange upya ili wakati mwingine yakitokea mashindano uwe umejiandaa vizuri zaidi kisaikolojia kwa ajili ya ushindi.
Tambua kuwa maadamu uko hai, hutakiwi kukata tamaa kabisa kwani hujui Mungu amekuwekea nini katika maisha yako. Hivyo kukata tamaa, iwe ni mwiko kabisa. Daima yakupasa usonge mbele.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection