Muosha Huoshwa!

Christina Mande
Wisdom&Wellness Counselor

Kizinga, Dar-es-Salaam

Mwosha kwa uelewa wangu ni mtu anayetumika kumwosha maiti na kumuandaa kwa mazishi. Zoezi hili la uoshaji hufanywa zaidi na watu wenye imani ya Dini ya Kiislamu. Kazi ya kuosha maiti huwa ni ngumu kidogo ndio maana inafanywa na watu maalumu. Na mwosha huyo naye akifa huoshwa vile vile na mwosha mwingine. Hayo ndiyo maisha yetu sisi wanadamu.

Tukirudi katika maisha yetu ya kila siku, mwosha ni mimi na wewe. Hebu tujiulize, je tunaishije na wenzetu? Katika familia, mahali pa kazi na katika jamii kwa ujumla, tunashirikianaje?Kama tunaishi kwa kutenda mema basi tutaheshimiwa. Lakini kama tunawatendea wenzetu maovu kwa kuwanenea mabaya, kuwasengenya kuwanyanyasa, kuwaonea n.k basi tujue yote yataturudia na riba kwetu. Kama sio kutoka kwao tuliowatendea, basi yatatoka juu kwa Muumba wetu ambaye Yeye huona kila kitu. Yatupasa tuishi kwa upendo na amani ili kuweza kupata baraka kutoka kwa Mola wetu

Previous
Previous

Asiyekubali Kushindwa, Si Mshindani!

Next
Next

Kuugua Siyo Kufa