Kuugua Siyo Kufa

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuugua ni hali ya kuwa na ugonjwa, na mtu mwenye ugonjwa hujulikana kama mgonjwa. Mtu anayeugua au mgonjwa hupenda kupata tiba ili aweze kupona. Mara nyingi mgonjwa anapozidiwa, fikra zinazomuujia ni kuwa anaondoka, yaani anakufa.
Wagonjwa wengi hufa kwa kukata tamaa. Wengi hujenga hofu, wasiwasi na mashaka juu ya afya zao. Wengine hufikia hatua ya hukiri kabisa kuwa wanakufa.
Msemo huu wa kuugua siyo kufa ni msemo wenye maana kubwa. Tunashauriwa kuwa tunapopata matibabu tuwe na ukiri chanya kuwa tutapona. Duniani ni mahali pa mapambano, iwe ni katika magonjwa uchumi, elimu, kilimo na ama ufugaji. Tusiwe watu wa kukata tamaa, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunakaribisha madhara makubwa. Madamu upo hapa duniani, yakupasa upambane katika kila nyaja.
Jipe moyo na matumaini ya kushinda. Watu wengi huugua na kupona. Mungu aliyekuleta duniani ndiye mwenye maamuzi juu ya maisha yako. Hivyo basi, “Kuugua sio kufa".
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection