
Muosha Huoshwa!
Mwosha kwa uelewa wangu ni mtu anayetumika kumwosha maiti na kumuandaa kwa mazishi. Zoezi hili la uoshaji hufanywa zaidi na watu wenye imani ya Dini ya Kiislamu. Kazi ya kuosha maiti huwa ni ngumu kidogo ndio maana inafanywa na watu maalumu. Na mwosha huyo naye akifa huoshwa vile vile na mwosha mwingine. Hayo ndiyo maisha yetu sisi wanadamu.

Mwiba Wa Leo Ndiyo Ua La Kesho!
Mwiba ni sehemu ya mti kwenye tawi ambayo lina ncha kali. Usipokuwa makini inaweza ikakuchoma.

Ndege Hai Hula Mchwa, Akifa Naye Huliwa Na Mchwa.
Ndege ni mkubwa kwa umbile ukimlinganisha na mchwa na sisimizi ndio maana anaweza kuwala wadudu hao bila shida. Lakini ndege huyo huyo akifa biashara inabadika. Akifa anakuwa hana ubabe tena, hivyo mchwa na sisimizi nao wanapata ubavu wa kumla.

Pakacha Kulivunja Nafuu Ya Mchukuzi!
Pakacha ni aina ya kapu litumikalo kubebea vitu. Mchukuzi wa kapu hili ni mtu anayebeba mizigo, aidha ikiwa ndani ya pakacha au chombo kingine. Pakacha likijaa vitu linaweza likawa zito lakini jinsi lilivyosukwa linaweza kuruhusu vitu vilivyowekwa humo ndani kuvuja au kumwagika kidogo kidogo wakati vimebebwa na hivyo kupungua kwa uzito ambao humpa ahueni mbebaji /mchukuzi.

Wembe Ni Mkali Lakini Haukati Mti, Shoka Ni Kali Lakini Haikati Nywele.
Wembe na shoka ni nyenzo zinazotumika kukatia vitu kwa mazingira tofauti. Kwa mfano, wembe unatumika kunyolea.nywele, kukatia kucha na vitu laini. Kwa vyovyote vile, wembe hauwezi kukata mti. Kwa upande mwingine, shoka ni kali na ni nzito lakini haliwezi kunyoa nywele.


MAHUSIANO MAZURI YANAYO RUHUSU MAJADILIANO
Mama Sixtha Komba (M&E Officer, TEWWY) atuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na uwanja wa majadiliano hasa kati ya vizazi.




