Pakacha Kulivunja Nafuu Ya Mchukuzi!

Christina Mande
Wisdom&Wellness Counselor
Kizinga, Dar-es-Salaam
Pakacha ni aina ya kapu litumikalo kubebea vitu. Mchukuzi wa kapu hili ni mtu anayebeba mizigo, aidha ikiwa ndani ya pakacha au chombo kingine. Pakacha likijaa vitu linaweza likawa zito lakini jinsi lilivyosukwa linaweza kuruhusu vitu vilivyowekwa humo ndani kuvuja au kumwagika kidogo kidogo wakati vimebebwa na hivyo kupungua kwa uzito ambao humpa ahueni mbebaji /mchukuzi.
Msemo huu unamaanisha, mathalani,
ndugu, rafiki au jirani yako akiwa na shughuli, mfano harusi, ugonjws au kitu kinachofanana na hivyo na hawajashirikisha majirani pamoja na wewe, yakupasa usijisikie vibaya kwa kuona kuwa wamekutenga.
Kiukweli kabisa, ni vema uchukulie kuwa wamekupunguzia mengi. Wangekushirkisha pengine ungetumia muda mwingi kwenye maandalizi ya hiyo shughuli. Na siyo hivyo tu, utajikuta unatakiwa kuchangia fedha na mambo mengine. Itakupasa wewe uendelee na kazi zako. Hii ndiyo inakuwa nafuu ya mchukuzi.