Unakimblia Wapi Unapopatwa Na Jambo?

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Yako mambo yanayotokea katika maisha ya mtu pasipo yeye mwenyewe kujua. Mambo hayo yanaweza yakawa mazuri au mabaya lakini pengine yeye haelewi nini kinaendelea.

Mtu akikutwa na mabaya anamshirikisha Mungu na watu wengine. Lakini pale anapokutwa na mambo mazuri, Mungu hawi kati ya wale ambao watashirikishwa. Yeye huona ameweza kupata hayo kutokana na akili yake mwenyewe.

Hebu na sisi tutafakari. Je sisi tulipopatwa na mambo mazuri tulienda wapi? Mathalani, baada ya kumpata mchumba ulimwambia nani? Au baada ya harusi yako ulienda wapi? Mlienda fungate au kanisani/msikitini kufurahi na Muumba wenu? Ni watu wachache wanapopata baraka hurudi na kufurahi na Muumba wao. Wengi wao hufurahi na wapenzi wao na wanasahau kumshukuru Mungu.

Je uliponunua gari , nyumba, au kiwanja ulifanya nini? Wengine waliita mchungaji au shekhe aje kuwawekea wakfu. Lakini wengine waliita marafiki ili wafurahi pamoja. Je ni nani alipiga goti na kumshukuru Muumba wake kwa baraka hizo alizojaliwa?

Mungu anatushangaa pale tunaposhindwa kushukuru pindi tunapofanikiwa. Vyovyote iwavyo, liwe jambo jema au baya hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kuwa ni mwema.

Sisi wana tewwy tunamshukuru Mungu kwa ajili ya uponyaji wa mnasihi mwenzetu ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda kidogo. Sifa na Utukufu tunamrudshia Yeye aliye juu. Binadamu tumeagizwa kuwa tushukuru kwa kila jambo, liwe zuri ama baya, lolote linalotupata katika maisha yetu

 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Pakacha Kulivunja Nafuu Ya Mchukuzi!

Next
Next

Utayari Una Faida.