BUSARA ZIANGUKIAZO KWENYE "T" TATU

Mama Sixtha Komba anatueleza juu ya T tatu ambazo unaweza tumia katika kuyakabili matatizo ukutananayo. Akianza na fafanuzi juu ya T tatu.
- T1 ni Tatizo
- T2 ni Tatuzi
- T3 ni Tokeo
Mama Sixtha Komba anaendelea kufafanua hizi T tatu katika nyanja mbili, hasi na chanya kwa kutumia mfano wa mwanafunzi aliyefeli mitihani yake na jinsi wazazi wanavyolipokea swala hilo.
Matumizi hasi ya T tatu
T1 ambayo ni Tatizo - Kijana kafeli mtihani
T2 ambayo ni Tatuzi - Wazazi/walezi wanamkasirikia na kuamua kumfukuza nyumbani
T3 ambayo ni Tokeo - Kijana anaingia mtaani na kujiingiza kwenye makundi mabaya kama uvutaji bangi, wizi, unywaji wa pombe kupita kiasi au kuamua kujidhuru.
Matumizi chanya ya T tatu
T1 ambayo ni Tatizo - Kijana kafeli mtihani
T2 ambayo ni Tatuzi - Wazazi/walezi wanaamua kumtia moyo kijana wao na kutaka kujua kwanini alifanya vibaya ili wamsaidie.
T3 ambayo ni Tokeo - Kijana baada ya kutiwa moyo na wazazi/walezi anaamua kurudi shule akiamini atafanya vizuri na atakuwa msaada katika jamii, kwani mti mmoja hauanguki mara mbili.
Contact Us
Don’t hesitate to reach out with the contact information below, or send a message using the form.
Tap Elderly Women's Wisdom for Youth
Tewwy, Jemedali St, Dar es Salaam, Tanzania
+255 737 773 982 | +255 757 327 878 tewwy@tewwy.org