Wembe Ni Mkali Lakini Haukati Mti, Shoka Ni Kali Lakini Haikati Nywele.

Christina Mande
Wisdom&Wellness Counselor
Kizinga, Dar-es-Salaam
Wembe na shoka ni nyenzo zinazotumika kukatia vitu kwa mazingira tofauti. Kwa mfano, wembe unatumika kunyolea.nywele, kukatia kucha na vitu laini. Kwa vyovyote vile, wembe hauwezi kukata mti. Kwa upande mwingine, shoka ni kali na ni nzito lakini haliwezi kunyoa nywele.
Msemo huu tukiupeleka katika maisha ya kila siku ya mwanadamu, unatufundisha kuheshimiana na kuthaminiana kwa sababu kila mmoja wetu anamtegemea mwingine. Kwa maana hiyo, kila mmoja wetu ana umuhimu kwa mwenzie, huo ndio uhalisia wenyewe.
Kwa mfano mtu anaweza kuwa mbobezi wa fani fulani. Mtu huyu tunaweza kumfananisha na shoka. Hata hivyo, ili mtu huyu aweze kutekeleza majukumu yake, atahitaji wasaidizi ambao tunaweza kuwafananisha na wembe.