JITAHIDI KUWA NA MARAFIKI WAZURI WENGI LAKINI AMINI WACHACHE WANAOKUFAA

Christina Mande
Wisdom&Wellness Counselor
Kizinga, Dar-es-Salaam
Marafiki wazuri watakuunga mkono kwa mambo yote mema unayofanya au unayofikiri kufanya na pia kutokushabikia kufanya maovu. Hawatasita kukuambia ukweli pale utakapofanya au kufikiria kufanya maovu na daima watakuelekeza njia inayofaa.