Mwiba Wa Leo Ndiyo Ua La Kesho!

Christina Mande
Wisdom&Wellness Counselor

Kizinga, Dar-es-Salaam

Mwiba ni sehemu ya mti kwenye tawi ambayo lina ncha kali. Usipokuwa makini inaweza ikakuchoma.

Ua nalo ni sehemu ya mti kwenye tawi ambalo huchanua na kutoa rangi mbalimbali na za kupendeza.

Msemo huu unatufundisha kuwa mafanikio huja baada ya kazi ngumu na misukosuko mingi. Kwa mfano, mchimba madini ni lazima afanye kazi ngumu ya yakupasua miamba na kwa kipindi kirefu hadi aje kupata mafanikio.

Mkulina vilevile lazima atumie nguvu nyingi kulima ili baadae aweze kupata mavuno mengi. Mfanya biashara hali kadhalika, lazima apitie misukosuko mingi hadi kufikia mafanikio.

Hivyo mwiba unafananishwa na kazi ngumu na misukosuko mingi. Ua nalo linafananishwa na mafanikio.

Previous
Previous

Usilie Mbele Ya Adui, Hata Kama Unahitaji Msaada Wake.

Next
Next

Omba Ufahamu Katika Maisha Yako!