Usilie Mbele Ya Adui, Hata Kama Unahitaji Msaada Wake.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kupata na kukosa ndio maisha ambayo kila binadamu anapitia kila iitwapo leo. Kusaidiana katika shida na raha ndio kiulimwengu. Hapo ndipo tunapoonyesha upendo wetu kati ya mtu na mtu.

Lakini kuna tabia ambayo imejengeka katika jamii zetu. Tabia hii ni ya kusemana vibaya pindi pale mtu mwingine anapokuwa na shida na akaomba msaada kutoka kwa mwingine.

Inatokea pale yule anayeombwa maaada analigeuza tukio hilo la kuombwa kwa kuifanya ni hadithi ya kutangaza kwa wengine. Wakati mwingine anatangaza kwa watu hata huo msaada wenyewe hajautoa.

Tabia hii ya kusemana siyo nzuri hata kidogo. Ieleweke kuwa hakuna mtu ambaye hatakaa aombe msaada kwa mwingine. Wahenga walinena, maisha ya mwanadamu ni yale ya kupanda na kushuka. Leo unaweza ukawa juu, kesho ukajikuta umeshuka. Umdhaniaye siye, leo anaweza kuwa ndiye kesho na akawa na msaada kwako. Kama binadamu, yatupasa tuache uadui na tupende kusaidiana. Inapobidi kusaidiana na uwezo tunakuwa nao, ni vema tukafanya hivyo kwani hayo ndio maisha yetu sote wanadamu.

Usemi huu unatufundisha kuangalia na kutafakari ni nani anaweza kupokea shida zako na akakusaidia kwa moyo wa upendo. Sio kila aliye mbele yako ni wa msaada kwako. Lakini pia tunajifunza na umuhimu wa kutoa msaada kwa wenzetu bila kutangaza kwa wengine. Maisha yanatakiwa yawe ya kusaidiana na siyo ya kusemana.

 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Maji Yakimwagika Hayazoleki!

Next
Next

Mwiba Wa Leo Ndiyo Ua La Kesho!