Omba Ufahamu Katika Maisha Yako!

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ufahamu ni kujua kipi ni kizuri kwako na kipi ni kizuri kwa jamii inayokuzunguka.Hali kadhalika, ufahamu ni kujua kipi ni kibaya kwako na kipi ni kibaya kwa binadamu wenzio ili uweze kukiepuka.
Mtu yeyote mwenye ufahamu hutembea katika haki. Hata kama kuna jambo baya, atalihukumu katika haki.
Katika maisha, inakupasa ujihukumu mwenyewe kwanza pale unapokuwa umekosea. Usisubiri watu wakuhukumu. Watu wengi wana tabia ya kupenda kuhukumu wenzao na sio kujihukumu wenyewe. Hapo ndipo vurugu na kutokuelewana kunapoanzia. Ni kawaida ya wanadamu kupenda kujitetea kwanza. Ukijua kujihukumu katika yale mabaya unayoyatenda, basi utabadilika. Utakuwa mtu wa kuheshimu kila apitae mbele yako.
Usipoweza kujihukumu mwenyewe hautakaa ubadilike, zaidi utawachukia wale ambao wanataka ubadilike. Ukweli ni kwamba, ukiwa na tabia hiyo, hautaishia popote zaidi ya kushindwa.
Hatua ya kupata ufahamu, huwa ni ngumu sana kuifikia. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kuna vikwazo vingi vya kukutoa katika ufahamu. Hapo ndipo panahitaji uvumilivu maana mambo mengine yatakuudhi na kukukatisha tamaa.
Ukibahatika kupata ufahamu, utakuwa umepata kila unachohitaji katika maisha yako. Kwa kawaida, Mungu humtumia mtu mwenye ufahamu na huyo ndiye atakaye sababisha upate kile ambacho umekuwa ukikitamani siku zote. Ili uwe na maisha mazuri, yakupasa uombe kutunukiwa ufahamu na hapo ndipo utakapopata amani.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection