Maarifa Na Hekima Ni Bora Kuliko Vitambulisho.

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maarifa na hekima vina thamani sana kuliko hicho unachokitafuta. Ukiwa na ufahamu na hekima una zaidi ya fedha. Hii ni kwa sababu ukiwa na huo ufahamu na hekima utafanikiwa kuwa tajiri. Hekima itakuongoza kupata kila unachohitaji katika maisha yako.
Utajiri sio vitu bali ni jinsi mtu ulivyo. Kutokana na vile ulivyo, hekima inaweza kukufanya wewe uwe tajiri na pia mtu mwenye ustawi. Lakini pia kwa jinsi ulivyo, hekima inaweza kusababisha uwe maskini. Kwa maana utajiri au umaskini unatoka ndani yako na sio nje. Hii inatokana na jinsi vile mtu unavyowaza na yale unayotamka kutoka ndani yako. Ukweli ni kwamba chochote utakachowaza ndicho utakachosema na ndicho kitakachokuwa katika maisha yako. Kumbuka, ukijinenea mabaya utapata mabaya, na ukijinenea mazuri ni dhahiri yatatokea mazuri
Ukitaka kufanikiwa katika maisha yako, badili namna yakuwaza na namna ya kutamka kwako. Sema unavyotaka kuwa sawasawa na vile ulivyosikia na ndivyo itakavyokuwa kwako.
Maarifa na hekima ni ufunguo katika kupata kwenye maisha ya mwanadamu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection