Maamuzi Yako Leo Ndiyo Mlango Wako Wa Kutokea Kesho!

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Kimaisha, binadamu tunapitia pilikapilika mbalimbali. Nyingine ni za furaha na wakati mwingine ni za huzuni zenye kukatisha tamaa.

Unapokutana na changamoto zinazokukatisha tamaa unatakiwa kukaa na kutafakari kwa kina. Baada ya hapo, unatakiwa kufanya maamuzi magumu. Pengine maamuzi utakayofanya yanaweza yasikubalike na watu wengine, lakini wewe kichwani kwako unakuwa na malengo yako pamoja na maamuzi ambayo unaona yana faida na mwelekeo kwako.

Maamuzi utakayoyaamua yanaweza kukufikisha viwango vingine, na hayo ndiyo maisha. Hali kadhalika, maamuzi hayo yanaweza kuwa ndio mlango wako wa kutokea kesho na hata ukaweza kupata mafanikio chanya.

Pamoja na maamuzi hayo magumu, usipende kuahirisha mambo yako kuwa utafanya kesho, bali uwe mtu wa kufanya maamuzi yako leo. Kuna msemo usemao, linalowezekana leo lisisubiri kesho.

Tunachojifunza hapa ni kuwa tusichoke wala kukata tamaa katika maisha. Kumbuka kwamba maamuzi yako yaliyo sahihi leo ndiyo mlango wako wa kutokea kesho.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Maarifa Na Hekima Ni Bora Kuliko Vitambulisho.

Next
Next

Ndege Hai Hula Mchwa, Akifa Naye Huliwa Na Mchwa.