Msuli Tembo Matokeo Sisimizi.

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Tembo ni mnyama mkubwa kuliko wote waishio porini. Kwa upande mwingine, sisimizi ni mdudu mdogo sana kiasi kwamba usipoangalia kwa makini, unaweza usimuone kwa jinsi alivyo mdogo.

Msemo huu unatuasa tusiweke nguvu kubwa sana kwenye biashara na ujenzi. Endapo unaamua kuweka nguvu kwenye sehemu ngeni ambayo huijui na maisha na kipato cha watu wa mahali hapo hukijui, na pengine, kipato cha watu wa mahali hapo ni kidogo, hapo utakuwa mtihani kwako. Mathalani, mtu kuweka mtaji wa mamilioni mahali ambapo wenyeji wa hapo wanapenda/wana uwezo wa kununua vitu vya shilingi mia mia tu. Pale atakapoweza kununua kitu chenye thamani ya shilingi mia tano, basi anaona ni cha thamani kubwa sana kwake. Hali kadhalika endapo pale unapowekeza wakazi wake ni wachache, hapo pia lazima utapata matokeo madogo sana mithili ya sisimizi. Tuwe waangalifu.

Yatupasa pale tunapotaka kufungua biashara tuangalie na kuzingatia mambo mengi maana mwisho wa yote tutaambulia matokeo yafananayo na sisimizi. Endapo hali itakuwa ya kihasara hasara hivyo itakufanya uchukie yote uliyowekeza pamoja na mahali ulipowekeza biashara yako. Umakini ni wa kuzingatia sana katika mambo yote tufanyayo. La sivyo tunaweza kuishia kupata majuto.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Damu Nzito Kuliko Maji!

Next
Next

Adui Mwombee Njaa.