Damu Nzito Kuliko Maji!

Caroline Swai - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Viumbe vyote vyenye uhai pamoja na wanyama vina damu. Damu ikikosekana viumbe hivi haviwezi kuishi. Maji pia ni muhimu katika maisha ya viumbe hai, lakini umuhimu wake ni mdogo ikilinganishwa na damu.

Kila mwanadammu huzaliwa akiwa na ndugu. Ni katika mkutadha huu ndipo tunaweza kutumia msemo huu. Hii inatokana na ukweli kwamba ndugu wanaweza wakafanyiana matendo maovu sana lakini wasiweze kuvunja undugu wao. Ndugu hutakiwa kushirikiana kwenye mambo yote, yawe ya shida au raha. Inaweza kutokea mmoja wa wana ndugu hao akajitenga kwa sababu moja ama nyingine. Akiwa amejitenga, hufanya mambo yake kivyake vyake tu bila kushirikisha wenzie. Inapotokea hivyo ndugu wengine huguswa na hivyo kuchukua muda mwingi kumshauri ili arudi kundini kwa ndugu zake.

Ndugu ni watu ambao siyo rahisi kuwatupilia mbali. Kuufuta undugu siyo kitu rahisi. Mtu anapomkuta ndugu yake yuko kwenye matatizo, siyo rahisi kumwacha aendelee kuwa katika hali hiyo. Hujitahidi kadri ya uwezo wake kumnasua kutoka kwenye matatizo yake. Ni kibinadamu kabisa kwa ndugu kusaidiana. Huu ni wajibu, hata kama waligombana naye siku za nyuma.

Kimsingi sisi wanadamu tunatakiwa kushikamana, kusaidiana, na zaidi ya yote yatupasa tupendane kwani upendo huvunja mabaya yote ambayo yangeweza kutokea baina yenu. Kama ndugu, yatupasa tuwe na mshikamano na tuaminiane kwa lengo la kuimarisha amani.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Mcheza Kwao Hutunzwa.

Next
Next

Msuli Tembo Matokeo Sisimizi.