Mcheza Kwao Hutunzwa.

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mcheza kwao ni mtu ambaye anajishughulisha sana na mambo yanayofanyika kwenye jumuiya yake. Kutunzwa ni kupewa tuzo/zawadi pale atakapofanikisha jambo. Kiubinadamu huwa ni jambo zuri kutambuliwa mchango wao pale mtu afanyapo vizuri, iwe ni kwenye jumuia, masomo, kilimo ama eneo la kazi. Hata katika familia, inatakiwa zawadi zitolewe kwa wana familia.
Hii ni muhimu sana kwa ajili ya kuwapa moyo wa kuendelea kufanya vizuri zaidi na zaidi. Kumtambua mtu kwa mchango wake kwenye jamii ni kitu kizuri sana na kinatakiwa kihamasishwe.
Kwenye makala hii huu tunafundishwa kuwa anayewatendea ndugu au jamii inayomzunguka mambo mema hakosi kupata fadhila toka kwao. Ni wajibu wetu kutenda mema kwa kuwa tunaishi na ndugu na jamii inayotuzunguka. Yatupasa tucheze kwetu ili tutunzwe. Wahenga walinena, ‘Matendo yanasema zaidi kuliko maneno’. Tunajifunza kutenda mambo ya baraka kwa jamii ili tuweze kutambulika na kutunzwa.sha. Tupendane kwani maisha ni mafupi.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection