Maneno Matupu Hayavunji Mfupa.

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maneno ni matamshi yaliyoandikwa ama yaliyotamkwa kutoka kwenye vinywa vya watu. Mathalani, maneno yanaposemwa juu yako ni budi ukayatafakari kwanza ili ujue yana maana gani. Endapo maneno hayo hayaleti madhara yoyote basi hayatakuwa na shida kwako, shida itakuwa pale tu mtu atakapokushikia silaha na akakudhuru.

Yatupasa tuyatafakari maneno yanayosemwa dhidi yetu. Lazima tujiulize, je maneno hayo yana lengo gani. Kama yamesemwa kwa ubaya na hayana ukweli wowote, yatupilie mbali. Hayo hayawezi kukudhuru. Ikumbukwe kuwa ni kawaida kwa mwanadamu yeyote kusemwa. Hata hivyo siyo vizuri kwa binadamu kuwasemea wenzao maneno yasiyofaa kwani wanaweza kuwasababishia wenzao msongo wa mawazo, kitu ambacho siyo kizuri.

Lakini pia tujifunze kudharau maneno yanayosemwa dhidi yetu na hasa pale yanapokuwa hayana msingi ama ukweli wowote. Kusemana ni kawaida, maisha ndivyo yalivyo.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Upandacho Ndicho Uvunacho.

Next
Next

Mcheza Kwao Hutunzwa.