Upandacho Ndicho Uvunacho.
Simulizi
by Caroline Swai (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Je ni kweli?
Fuatana nami katika simulizi hii.
Katika kijiji kimoja alikuwepo mfanya biashara mmoja aliyekuwa akiuza siagi. Mfanya biashara huyu alikuwa na mteja wake maalum mjini ambaye alikuwa na duka kubwa la vyakula. Hawa wawili walikuwa na makubaliano ya kubadilishana bidhaa. Makubaliano hayo yalikuwa hivi: siagi katika vifungashio vya kilo moja moja,kwa bidhaa za vyakula tofauti tofauti. Kwa maana hiyo, wafanya biashara hawa wawili walikuwa hawauziani bali wanabadilishana kufuatana na makubaliano yao.
Siku moja mwenye duka aliamua kupima vifungashio vyote vya siagi. Cha kushangaza, alikuta kila kifungashio kina uzito wa gramu 900 badala ya kilo moja waliyokuwa wamekubaliana. Alikasirika sana. Alifura mno kwa hasira Isitoshe kifani.
Kama kawaida, muuza siagi alileta tena siagi hapo dukani. Mwenye duka alipomuona tu, bila kuchelea, alimwambia, “tafadhali ondoka dukani kwangu kwani umekuwa
ukinipunja gramu 100 kwa kila kilo moja ya siagi. Sitaki kukuona tena hapa,” aliendelea kubwabwaja maneno yake ya hasira.
Naye muuza siagi alijitetea na kusema, “Bwana wangu, mimi ni masikini sana kiasi kwamba siwezi kununua hata mawe ya mizani ya kupimia siagi. Hivyo huwa naweka kilo moja ya sukari unayonipa upande mmoja wa mizani na kupima siagi upande mwingine. Kwa hiyo ina maana kuwa, hata wewe kila bidhaa unayonipa ina uzito wa gramu 900, sawa na siagi nikuleteayo”.
Kwa hakika, hapo ilikuwa ngoma droo.
Tunajifunza nini hapa? Hapa tunaaswa kutomtendea mtu mwingine jambo ambalo sisi tusingependa kutendewa. Wahenga walinena, “Mtenda hutendewa”.
Tumeyaona kwenye simulizi hii
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection