Unaweza Kusahau Maumivu Lakini Sio Tukio!

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Unaweza ukawa na maumivu fulani kama ni ya ugonjwa au maumivu mengine ya maisha. Maumivu hayo yanaweza kuwa ni ya muda fulani au kipindi fulani tu lakini mwisho yakapata jawabu. Katika hali hiyo unaweza ukasahau tu pindi pale linapokuja kupata majibu. Hapo itakuwa sio rahisi tena kukumbuka kama kuna jambo lilikuwa limekutesa. Mfano mzuri ni pale unapokuwa unaumwa lakini ukipona inakuwa sio rahisi tena kukumbuka maumivu uliyokuwa ukipata.
Ndivyo ilivyo katika maisha ya kila siku.
Inapokuja kwenye tukio jingine, hiyo inakuwa ni kama kovu ambalo linakupa kumbukizi kila unapoliona. Matukio mengi huwa yanakumbukwa sana kutokana na wepesi na uzito wake pia. Maana hata kama mtu alikufanyia jambo baya kila utakapomuona utakumbuka kile alichokutendea.
Matukio yanakaa sana kwenye kumbukumbu za watu. Tukio huwa linajitangaza lenyewe kutokana na uzito wake. Matukio hutengeneza historia kwa wakati husika.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection