Bidii Ina Tabia Ya Kumtabulisha Mtu.

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Watu wengi tunafanya mambo lakini hatuyafanyi kwa bidii, tunafanya ili mradi tu yafanyike. Unaenda kazini lakini huna bidii ya kwenda kazini, leo unaenda kesho hauendi. Kila siku unaenda ukiwa wa mwisho na unatoka ukiwa wa kwanza.
Umeanzisha biashara fulani lakini leo wateja wakija wanakuta bidhaa kesho hazipo, unawambia huna bidhaa. Ukweli ni kwamba huna bidii kwa hilo unalolifanya, na pasipo kuwa na bidii, hakuna ubora.
Wengi wetu hatufanikiwi
kwa sababu mambo mengi tumeyafanya kwa mkono mlegevu.
Ukiwa na bidii katika kazi yako au kwa hilo unalofanya iko siku kazi hiyo itakutambulisha kwa wakuu na kukupeleka mahali ambapo hukutegemea.
Kuna watu wanakutazama sasa na hilo unalolifanya na ipo siku hao hao watu watakupendekeza kwa watu wakuu na mambo yako yakakunyookea.
Huwezi kujua unayemhudumia leo ni nani, hivyo toa huduma nzuri kwa watu wote. Haijalishi kama wewe ni mama wa nyumbani, umeajiriwa au umejiajiri, tia bidii katika hilo ulifanyalo.
Hebu nikuhamasishe kidogo. Mwaka huu wa 2024 nakushauri ufanye maazimio ya kuwa na bidii, ongeza bidii katika kila eneo la maisha yako. Utakuja kuona mafanikio ambayo hukuyataraja.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection