Usiache Tawi Kabla Hujashika Tawi!

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Matawi ni sehemu ya mti ambayo huchipua katika mti na ile sehemu inayoshika majani. Ni kawaida ya mtu ambaye anapanda au anashuka mtini kushika tawi, asipofanya hivyo anaweza kuanguka.
Msemo huu una maana kubwa sana. Mfano mtu kukosolewa tu anachelewa kazini, au kuonywa kwa mdomo kuwa tabia aliyonayo aache mara moja anahamaki na kutaka kuacha kazi, akitegemea atapata kazi nyingine. Uamuzi wa namna hii hautakiwi. Kinachotakiwa hapa ni uvumilivu. Inampasa mtu atafute kazi mahali pengine, pale atakapopata ndipo anaweza kuacha kazi mahali ambapo anaona pana usumbufu. Hatutakiwi kuacha kazi kabla hatujapata kazi nyingine.
Hapa tunajifunza kuwa kwanza pata kitu cha kufanya kabla hujafanya maamuzi ya kuondoka pale ulipokuwa mwanzo. Maamuzi ya pupa huleta hasara.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection