Jifunze Kutangaza Mema Kwa Ajili Yako.

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Mara zote unatakiwa kutangaza mema kwa ajili yako. Kila mara jiambie, mimi sio wa kushindwa kwa sababu sikuumbwa kushindwa.
Uliumbwa kushinda na sio kushindwa kwenye mambo yote yawayo. Mara nyingi huwa tunakata tamaa pale tunapokutana na magumu. Usiongee madhaifu yako kwa watu bali weka siri ya mambo yako. Tangaza ushindi wako. Kumbuka jinsi unavyotangaza, ndivyo unavyowezesha mambo yako yatokee.
Kamwe usitangaze maumivu yako. Jifunze kutangaza mazuri yako hata kama hayajatokea. Kuwa na imani na kitakachokuja. Kama ilishindikana jana, tegemea kesho yako itakuwa njema. Mathalani, kama biashara haijaenda vizuri leo, yakupasa ushukuru huku ukijua kuna kesho pia.
Tunashindwa pale tunapoanza kushirikishana maneno hasi. Inawezekana kweli mwenzio kashindwa, lakini hiyo ni yake yeye. asikushirikishe kushindwa kwake. Kushindwa kwake yeye sio kushindwa kwako wewe, wala shida zake yeye siyo shida zako wewe. Unapotangaza kushindwa ni kama unamwarisha yule aliye juu aje kukupa usaidizi.
Yakupasa ujipende mwenyewe, usingoje mtu mwingine aseme kuwa anakupenda.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection











