Njia Ya Muongo Ni Fupi!

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Mwongo ni mtu ambaye huwa hasemi ukweli. Mtu wa namna hii mara nyingi huwa ni mzungumzaji sana, hakosagi maneno ya kusema kabisa.

Msemo huu hugusa watu wengi kwa sababu mtu mwongo kutokana na usemaji wake, huwa ni msahaulifu. Mtu wa aina hii huwa hakumbuki alichokisema. Baada ya muda mfupi tu huweza kukueleza kitu kile kile ambacho tayari alikuwa amekwishakueleza. Hujichanganya sana na hiyo ndio inakuwa ishara kubwa ya uongo wake kwenye jamii.

Wahenga walisema ukiwa mwongo inakupasa uwe na kumbukumbu sana, na pia Uwe na akili. Yakupasa ukumbuke vizuri kile unachosema leo ili kisije tofautiana na kile utakachosema kesho. Mtu mwongo lazima awe na kumbukumbu kali la sivyo uongo wake utakuja kumuumbua siku moja.

Mtu mwongo huweza danganya maisha ya hapa duniani tu. Lakini yatupasa tukumbuke kuwa hatuwezi kuishi kwa kudanganya maana siku moja mambo yote yatajulikana tu. Daima tukumbuke kuwa maisha ya ukweli ni maisha maisha ya afya, na hii ni pamoja na afya zetu za akili.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Bora Lawama Kuliko Fedheha!

Next
Next

Tunda Jema Halikai Mtini.