Usisumbuke Na Wanao Sumbuka Na Wewe!

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Wapo watu ambao maisha yao siku zote huwa wanatafuta habari za wenzao, wao hawana lingine. Mara nyingi habari zenyewe huwa ni za kuwachafua tu wenzao. Watu kama hawa, mara zote hupenda kuwanenea wenzao mabaya Kwa malengo ya kuwafanya waonekane si kitu mbele za watu. Yote hii ni kwa sababu ya roho mbaya walizokuwa nazo, hakuna jingine zaidi. Mapenzi yao makubwa ni kuona wenzao wanaonekana vibaya mbele ya kadamnasi.
Usemi huu unatufundisha kutokujali yale yasemwayo juu yetu na hasa kama hakuna ukweli ndani yake. Watu huwa hawachoki kusema wenzao, hii ni tabia ya binadamu walio wengi. Pale unapoingia unasakamwa na maneno, hebu jaribu kujiambia kuwa ‘watasema mchana, usiku watalala.’ Yaruhusu maneno yaingie sikio la kulia na yaache yatokee sikio la kushoto. Acha waseme.
Watu wakikusema, wewe songa mbele. Waache wajicheleweshe wenyewe. Watakapokuja kushituka, watakukuta wewe uko mbali. Acha wale wanaosumbuka juu yako wasikusumbue na wewe. Daima mbele, nyuma mwiko.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection