Taulo Sio Vazi La Kucheza Na Watoto

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwa kadri maisha yanavyokwenda, umakini unatakiwa uzingatiwe sana. Maana jana ikipita hairudi tena. Utabaki unajutia tu jinsi wakati unavyokwenda. Utafikia mahali utajisikia vibaya kwa jinsi hali yako inavyozidi kuwa ngumu na mbaya.
Utabakia kujisemea tu kuwa mimi nilikuwa hivi ama vile. Maskini, wakati huo hakuna atakaekuelewa, hata kama alishuhudia vile ilivyokuwa, yaani vile ulivyokuwa hali yako ya zamani. Watabaki kukucheka tu huku nawe ukibaki unaona aibu.
Usemi huu unatufundisha kuwa makini na muda maana usipokuwa makini utajikuta umechezea muda ambao huwezi kuurudisha. Sawasawa na taulo ambayo inaweza kukuvuka ukicheza na watoto watakucheka nawe utapata aibu ambayo huwezi kuifuta.
Tuzingatie muda na wakati katika mikakati yetu ya maisha. Linalowezekana leo lisingoje kesho. Kesho ina mambo yake na ratiba zake tofauti na leo. Tusikumbuke yaliyopita, tuangalie yaliyopo sasa na yajayo, muda sio rafiki kwetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection