Ishi Kwa Amani Na Furaha

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Maisha yakikupa sababu mia moja za kutokuwa na furaha, wewe yape sababu elfu moja za kuwa na furaha.

Maisha yana mambo mengi na vitu vingi vinavyoweza kutunyima amani na kuiba furaha zetu. Hata majira ambayo kwako sio sababu ya kukosa amani, adui atatumia vitu au watu kuiiba furaha yako.

Hivyo ukitafuta furaha kulingana na mazingira au hali fulani, yumkini maisha yako yote ukaishi bila kuwa na amani wala furaha, njia pekee ya kukusaidia kuja kuwa mtu mwenye furaha ni kuamua kuwa na furaha kutoka ndani ya moyo wako na sio kwa kuangalia mazingira au hali unayopitia.

Jifunze kufurahi hata kwenye mazingira ambayo adui anajua huwezi kufurahi, mazingira ambayo adui anajua amekukomesha au kukuweza. Wewe mchekee tu, muonyeshe hadi jino lako la mwisho. Kamwe, usionyeshe dalili ya kuridhia yale yanayokukabili kwa wakati huo. Simama imara, usiyumbe wala kutetereka.

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Taulo Sio Vazi La Kucheza Na Watoto

Next
Next

Tatizo Huzaa Faida.