Tatizo Huzaa Faida.

Simulizi
by Victoria Nakajumo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Tatizo ni tatizo, liwe la afya au la uchumi, mwisho wake litazaa faida. Hata likiwa ni tatizo la madeni, bado nalo litazaa faida. Kila tatizo lako litazaa faida katika maisha yako kwa sababu, kila tatizo lililo mbele yako, katika hali ya kawaida, utalifanyia kazi na mwisho kutakuwa na faida.
Kanuni ya msingi ni kwamba ili uweze kupata faida ya tatizo lako ni kuondoa uoga l, kwa maana iliyo wazi kabisa, usiogope.
Mfano mdogo ni pale mtu anapodiriki kusema kuwa hawezi kuruka. Lakini akitokea Simba aungurume tu, huyo huyo aliyesema hawezi kuruka ndio atakuwa wa kwanza kuruka ng'ambo ya barabara.
Kama binadamu, inatupasa tuelewe kuwa matatizo yetu huishia kwenye mafanikio na pia kuna ushindi wetu, tuache kuogopa. Kuna ushahidi mwingi tu unaoonyesha kuwa watu wengi walioinuka kimaisha walipitia matatizo mengi na walijikuta hatimaye wakiwa na mafanikio makubwa. Hatupaswi kuogopa pale tunapokumbwa na matatizo, yatupasa tutafute kila njia ya kushinda ili tuweze kupata ujira mbeleni.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection