Timiza Leo Yako Ili Kuifanya Kesho Yako Iwe Bora.

Alfreda George - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Sijui wewe unatimizaje siku yako. Unaweza ukawa unalalamika kuhusu watoto wako lakini unapaswa kujiuliza wewe mwenyewe kwanza endapo umetimiza ipasavyo kwa ajili ya yale unayoyataka kwa ajili ya watoto wako.

Kwa kawaida mtu huvuna alichopanda. Leo hii unapolalamika kuhusu watoto wako kutokukuelewa, ni vema ukajiuliza kwanza wewe mwenyewe, kile uluchopanda kwa ajili ya watoto wako hao. Kumbuka, ya jana huwa hayarudi.
Furaha yako leo itategemea sana na maandalizi yako ya jana.

Wengi tunatamani tuwe na maisha mazuri na kipato kiwe kizuri. Swali ni lile lile, kuhusu ulichopanda jana ili kuwezesha kipato chako kiwe kizuri leo.

Kama unataka kesho yako iwe nzuri anza kuifanyia maandalizi leo. Kama unataka watu wakupende na upate kibali machoni pa wengi, kumbuka kupanda mazuri leo yako.

Kama huoni jinsi ya kukipata unachotamani, basi amua leo kufanya vyema ili uweze kutimiza azma yako siku ya leo na uweze kuifurahia kesho yako. Maandalizi mazuri ya maisha yanatokana na jinsi ulivyojiandalia, hakuna muujiza wowote. 

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Tatizo Huzaa Faida.

Next
Next

Ukitaka Ubaya, Dai Chako