Ukitaka Ubaya, Dai Chako

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Usemi huu unaendana na ule usemao kukopa harusi kulipa matanga. Kuna tabia ambayo imejengeka katika jamii zetu ya kusaidiana kupitia kukopeshana. Mtu anapokuwa na shida anakuja kwa machozi na heshima zote na kuweka tarehe ya kurudisha. Hata kama mkifikia kuandikishana mkataba, huwa yuko tayari. Tatizo linakuja pale muda wa kurudisha unapokuwa umepita.
Ukimkumbusha atakupatia ahadi nyingi na mwisho wake ni kuanza kukusema vibaya. Utamsikia akisema, jamaa ananidai, vihela vyenyewe vidogo tu, yaani ananikera kweli kweli. Cha ajabu, amesahai kuwa alikuja kwako huku akilia, mikono nyuma.
Eti sasa anaona ni kidogo alichokopa. Kama ni kidogo mbona hakuwa nacho wakati ule? Hapo ndipo visa vinaanza na uadui wa kutengeneza unaanza. Kama hiyo haitoshi, utatangaziwa ubaya kwa kila mtu ili watu wakuone wewe mbaya.
Hayo ndio matokeo ya kudai chako. Ulimkopesha kwa sababu ya uungwana wako na moyo wa kusaidia. Ukweli ni kwamba kuna watu ambao ni wepesi sana wa kukopa lakini ni wagumu sana wa kurudisha. Ni vizuri kama una shida, kopa lakini yakupasa ulipe ili uweze kuendelea kuaminika na uwe na amani moyoni mwako. Kulipa deni ni ubinadamu ambao yatupasa tuzingatie. Wengi ubinadamu huo hawana. Watu wa namna hii wanaaswa kubadilika.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection