Ukitaka Kushindwa Katika Maisha, Mshirikishe Ndugu

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Maisha yetu sisi binadamu yamezungukwa na mambo mengi na pia na jamii tofauti tofauti. Unaweza kuishi kwenye jamii fulani na ukaona mambo yako yanakuendea vizuri sana. Kutokana na kuwa katika hali hiyo ya kuona mambo yako yanakwenda vizuri, unaweza ukaamini kuwa uko katika usalama.
Wakati huo huo pia una ndugu ambao wanakuzunguka. Unaweza kuwa na shughuli zako unazozifanya, ukaona pengine umshirikishe ndugu yako ili mambo yawe mazuri zaidi. Hapo unakuwa unaamini kuwa kwa vile ni ndugu yako atakuwa na uchungu na shughuli yako kwa vile inamhusu na yeye pia, kwa njia moja au nyingine.
Kubali usikubali, huyo ndugu yako uliyemuamini utakuja kujikuta amekuangusha vibaya sana. Utabaki unajuta, bora ungemshirikisha mtu baki, mtu ambaye sio ndugu yako anayeweza akaheshimu kazi yako na akakufanyia vizuri kuliko ndugu yako.
Ukweli ni kwamba ndugu anajua kuwa hata akikufilisi, udugu wenu utabaki pale pale kwa kuamini kuwa damu ni nzito kuliko maji.
Usemi huu unatufundisha kuwa makini na hao tunaowaita ndugu zetu. Ni vema tusiwashirikishe kwenye mambo yetu. Ukweli unaonyesha kuwa mara nyingi atakayekuangusha ni mtu wa karibu yako. Ni lazima tujihadhari sana kufanya biashara ama vitu vyovyote vya maendeleo na ndugu zetu. Wengi hawaaminiki kwa sababu wanajivunia mahusiano yaliyopo baina yenu. Kwa hakika, inasikitisha, tuwe waangalifu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection