Akiba Haiozi

Grace Mshanga - Wisdom&Wellness Counselor (TEWWY)

Simulizi

by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).

Akiba ni kitu chochote kinachowekwa kwa ajili ya matumizi ya baadae. Neno haiozi, lina maana ya kutoharibika au kuokufaa kwa matumizi.

Akiba haiozi ni msemo ambao unatukumbusha kuwa katika maisha ya mwanadamu, kuna matumizi mengi sana . Lakini katika matumizi hayo mengi, ni budi kujiwekea akiba mara kwa mara ili baadae iweze kukusaidia pale utakapopambana na shida.

Tunaposema akiba haiozi tunamaanisha kuwa wakati wa dharura kama vile magonjwa, kifo ama kuunguliwa nyumba, akiba uliyojiwekea huko nyuma inaweza kukusaidia sana wakati huo.

Hakuna akiba mbayo inaharibika, bali humsaidia mtu kutatua changamoto ambazo zimeweza kutokea bila kutegemewa.

Sote tunajua, majanga, dharura na changamoto nyingine nyingi hutokea kwa wanadamu. Hivyo yatupasa tujifunze kuweka akiba mara kwa mara katika maisha yetu. Hii itatusaidia, pale tunapopatwa na shida ama changamoto yoyote ile, tusikimbilie kwa watu huku tukilia tukiomba misaada. Ni budi tujiwekee akiba ili kukwepa adha za mahangaiko kwa sababu utakachojiwekea kama akiba, hakitaoza

The Healing Hands Project

The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection

Previous
Previous

Ukitaka Kushindwa Katika Maisha, Mshirikishe Ndugu

Next
Next

Cheo Ni Dhamana