Cheo Ni Dhamana

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Cheo ni wadhifa ambao mtu hupewa mahali pa kazi, katika familia, au katika jamii ili kutimiza majukumu kwa lengo la kuwaletea watu wa chini yake maendeleo.
Dhamana ni hali ya kuaminiwa katika cheo alichopewa mtu kwa vile ana uwezo wa kutekeleza mambo kwa ubora zaidi kuliko watu wengine.
Msemo huu ni wa muhimu sana kwetu sote wandamu. Wengi wanaopewa cheo au kuchaguliwa kushika nyadhifa fulani au madaraka, huwa wanajisahau. Badala ya kuwa wabunifu na kuboresha huduma au kazi zao zaidi, wanakuwa wanyanyasaji au waombaji wa rushwa na takrima kutoka kwa watu walio chini yao. Watu hawa wanapingana na usemi huu.
Msemo huu unamhusu mtu aliyepata cheo. Mtu huyu anatakiwa kuwajibika na kuboresha mfumo wa kazi ili uwe na tija zaidi kwa watu walio chini yake. Watu walio chini yake, wanatakiwa kunufaika na cheo chake na si vinginevyo.
Hali kadhalika, tunajufunza kuwa inatupasa tuwe wazalendo, tuipende nchi yetu pamoja na watu wake. Cheo cha mtu kitakuwa na uzuri pale tu kitakapokuwa na manufaa kwa watu watu walio chini yake.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection