Mwacha Asili Mtumwa

Simulizi
by Alfreda George (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Asili ya mtu yeyote ni chimbuko lake, yaani kule alikotoka. Chimbuko ama asili ya mwanadamu ni kitu muhimu sana katika maisha yake.
Alikozaliwa mtu ndiko unaweza kupata taarifa zake pamoja na kumbukumbu zake zote.
Mtu mwingine akishasoma au kupata maisha mazuri basi hudharau na kusahau kabisa asili yake. Husahau kule alikotoka. Wengine hudiriki hata kuona kuwa hali ya kule kwao haiendani na hadhi yake tena. Hujiona haendani na mazingira ya kule alikozaliwa.
Hali hii inapotokea huwa ni hatari sana. Huweza kuleta mtafaruku kwenye familia ya muhusika na hata kule alikozaliwa. Mazingira huwa magumu zaidi pale muhusika mkuu anapotangulia mbele za haki. Huiacha familia yake njia panda.
Hapa tunajifunza kuwa kila mtu anatakiwa kuthamini kule alikotoka. Huko ndiko chimbuko lake ambako kulimtengenezs awe vile alivyo. Yatupasa tuendelee kulinda na kuheshimu mambo yanayohusiana na kule tulikotoka, badala ya kukumbatia mambo yasiyokuwa asili yetu.
Tuheshimu, tutunze, tuenzi, tuthamini, na tuwe tunatembelea makwetu mara kwa mara ili kujenga mahusiano ya karibu na ndugu zetu katika chimbuko letu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection