Mbwa Ukimjua Jina Hakusumbui

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kwa kawaida, kila mtu anayo tabia yake ambayo mwingine hana. Huwezi ukamfananisha mtu na mtu mwingine katika nyanja yeyote ile. Binadamu tumeumbwa kila mtu kwa namna yake. Inawezekana kabisa kile unachokitaka wewe, mwingine asikipende, hivyo ndivyo maisha yanavyokwenda.
Lakini Mungu ametuumba ili tutegemeane. Kwa kadri unavyomuelewa mwenzio, ndivyo itakavyokuwa rahisi kuendana naye na pia kuelewa jinsi yeye anavyoelekea. Tujitahidi kuvumiliana ili tuwe na amani kati yetu.
Simulizi hii tunaweza kuipeleka kwenye mahusiano ya kiofisi pia. Ukimjua bosi wako vile anavyotaka utakuwa na amani hapo kazini. Hata kazi zako utafanya kwa uhuru zaidi kutokana na kumjua mkubwa wako. Lakini tabia ya kufanya kazi kwa uhuru kutokana na kumjua bosi siyo kitu kizuri kwani wale wasiokuwa na watu wanaowajua, watakuwa hawatendewi haki. Wao watakuwa hawana mahali pa kukimbilia pale wanapopata shida ya kikazi.
Lakini tunapenda kuwaasa wale ambao wanatumia mahusiano yao na mabosi kudharau wengine ambao hawana. Hata kama bosi ni jamaa yako, yakupasa ufanye kazi vizuri na kuwa na utii katika utekelezaji wa kazi zako. Kuheshimu mamlaka iliyopo ni wajibu wa kila mtu. Haijalishi kuwa wewe una mahusiano na bosi wako, bali ni kuwa na umakini katika kutii mamlaka iliyo juu yako. Huo ndio utaratibu unaofaa na unatakiwa kufuatwa.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection