Usikatae Wito, Kataa Neno

Simulizi
by Grace Mshanga (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Kuna wakati mwingine watu hufanya maamuzi ya jambo fulani bila kutafuta ukweli wa jambo hilo aliloambiwa. Inawezekana jambo aliloambiwa halina ukweli wowote ila kwa sababu ameambiwa na rafiki au jamaa yake wa karibu basi anajua hilo jambo litakuwa sahihi.
Ni jambo la busara sana pale unapoambiwa jambo kulifanyia utafiti kwanza. Kuchukua hatua ya kulichunguza jambo itasaidia kutoa maamuzi yaliyo sahihi. Yakupasa usikilize neno kwanza, lichambue na kulipembua ili kupata uhakika wa jambo. Tusipende kutoa hukumu bila kulitendea kazi jambo lenyewe. Endapo utashindwa kufanya hivyo, uhasama usiopingika baina yenu utatokea.
Hapo hapo, inakupasa uzingatie umuhimu wa kutokumkatisha tamaa yule aliyekuletea jambo. Wewe msikilize tu, kama unaona jambo lenyewe halina mashiko, basi liache. Usilikatae jambo lake bali jaribu kumsikiliza na ndipo uweze kulitolea maamuzi. Kama binadamu inatupasa kutumia busara wakati wote. Tunajua kuwa siyo rahisi kufanya hivyo, lakini inatupasa kujaribu. Tukifanya hivyo, itatusaidia kuishi vizuri na watu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection