Ubaya Ni Akiba Na Wema Ni Akiba!

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Ni jambo dhahiri kuwa watu tunaishi kwa kutofautiana tabia zetu tokea utoto wetu hadi ukubwani. Jamii huwa inasoma makuzi ya familia zetu kuanzia udogoni hadi unapokuwa mtu mzima. Huchunguza matendo na maneno yatokayo midomono mwetu. Tabia ambayo unaionyesha ndicho kinakuwa kielezo tosha cha wewe kujiwekea akiba ya ubaya au akiba ya wema.
Mara nyingi katika makuzi yetu, unapoanza kujitambua ndipo unapoanza kupata historia yako ya utotoni ambayo ulijiwekea akiba. Utasikia mara nyingi wanazungumza kuwa mtoto wa fulani alipokuwa mdogo alikuwa na maringo, kiburi, jeuri na mwenye dharau, lakini sasa hivi kabadilika. Amekuwa na heshima, mnyenyekevu na tena mwenye upendo kwa watu.
Hapo tunaanza kuona kuwa katika mabadiliko yako, watu wanataja kwanza akiba ya abaya wako ambao ulijiwekea mwenyewe, ndipo waelezee akiba ya wema wako. Yatupasa tuelewe kuwa jamii ni kioo cha maisha yetu. Tumejionea wenyewe kuwa mara nyingi, ubaya wote unafutwa na wema ambao kwa sasa jamii inakuwa imeridhia mabadiliko yako.
Kutokana na somo hili tunajifunza kuwa kila jambo tulifanyalo hutiliwa maanani na hutoa picha kamili ya mwenendo wako wa maisha. Unapofanya mambo yako, yawe mazuri ama mabaya, wewe unaweza kuyaona yamekwisha ama yamepita, lakini jamii huwa inajiwekea kumbukumbu ambayo itakuwa na kielelezo kibaya au kizuri katika maisha yako ya baadae. Tukitaka kuacha kumbukumbu safi, yatupasa tutende matendo yaliyonyooka ili jamii yetu inayotuzunguka iweze kuwa na hifadhi nzuri ya matendo yetu.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection