Ishi Kwa Viwango Ulivyojaliwa

Simulizi
by Margaret Kayombo (Wisdom&Wellness Counselor - TEWWY).
Katika maisha ya mwanadamu hapa duniani, Mungu amemjalia kila mtu karama na vipawa kwa biwango anavyostahili. Kutoka Hali hiyo, tunashuhudia kwenye jamii zetu kila mtu anafanya vitu tofauti na mwingine, pengine vinaweza vikafanana kwa kiwango kidogo tu.
Kuna wakati inatokea watu wanaingilia ama kuiga mambo yanayofanywa na watu wengine. Mwisho wa kuiga iga mambo ya wengine huwa siyo
mzuri ama huwa hawaambulii chochote. Matokeo yake huwa ni kupata hasara kubwa ambayo hupelekea kukata tamaa na hata kushindwa kusonga mbele.
Tunaona kwenye jamii watu huangalia mafanikio ya watu, mathalani, yule kafanikiwa kwenye biashara fulani basi naye atafanya kila mbinu ili amzidi kwa lengo hata ya kumharibia biashara yake. Kuna msemo unasema Mungu si Athumani. Utashangaa, pamoja na mbwembwe zote atakazozionyesha, bado huyo huyo fulani aliyelengwa kuharibiwa biashara yake, anazidi kupata mafanikio zaidi.
Hii yote inatokana na vile viwango ambavyo kila mtu amejaliwa na Muumba. Ukweli ni kwamba, hapo ni jinsi unavyovitumia vipawa vyake, na si vinginevyo. Endapo utavitumia kwa kumkomoa ama kumharibia mwenzio, ni lazima ujue kuwa ndiyo unajiharibia wewe mwenyewe. Mwisho wake unaweza hata ukajiharibia mahusiano yako na jamii inayokuzunguka. Watu watatu shanga na kukuona hufai.
Kutokana na maelezo hayo, tunajifunza kutopenda kuiga vitu ambavyo hatuna uwezo navyo. Yakupasa ufanye kile ulichojaliwa na Muumba wako. Hali kadhalika,
tunatakiwa kumuomba Mungu atuongoze kutenda yanayofaa, kuliko kutumia nguvu zaidi ya yale tuliyojaliwa. Kila mtu ana kitu cha pekee ndani yake ambacho mtu mwingine hana. Jifunze kuridhika na hali yako huku ukifanya kazi kwa bidii zako zote.
The Healing Hands Project
The Healing Hands empowers people to achieve financial autonomy by building entrepreneurial skills and embedding skills transfer within the community – alleviating poverty as a driver of ill mental health. Funds raised from the jewelry will help sustain free mental health services in underserved communities and promote the economic empowerment of trained grandmothers who implementing #WHO #mhGAP evidence-based psychosocial interventions. The project provides interpersonal counseling, group talk therapy, and psychoeducation resources, referrals, advocacy and awareness raising delivered through arts. Clients learn to handcraft traditional beaded jewelry as a marketable skill. Follow us @TEWWYWisdom @WisdomWellnessCollection









